ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 11, 2012

LICHA YA ZUIO LA POLISI WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAANDAMANA KULAANI MAUAJI YA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI, MPC YATOA TAMKO ZITO KWA RAIS JK.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC) Deus Bugaywa akisoma barua ya zuio la polisi kufanyika kwa maandamao hayo ya wanahabari kwa jiji la Mwanza ili kupisha ziara ya Waziri Mkuu sababu ambazo hazikuafikiwa na waandishi wote nao wakaendelea na zoezi la kuandamana kutoka viwanja vya Ghand hall jijini Mwanza na kupita barabara kadhaa hadi uwanja wa Nyamagana jijini hapa.
Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza (MPC) kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha kinyama cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi akiwa mikononi mwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa.

Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini september 2,2012 katika moikono ya polisi waliokuwa katika kazi maalum huko Nyololo, Iringa.

"BAADA YA MWANGOSI NANI ATAFUATA?"
Mauaji ya Mwangosi yamebadili sura ya Tanzania kimataifa kuwa ni kisiwa cha amani na sasa kuwa ni kisiwa cha mauaji, kwani Mwangosi amekuwa ni mwanahabari wa 38 kufa akiwa kazini kuanzia mwezi Januari 2012 hadi september 2012 Duniani, na haya ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi kufa akiwa kazini.

MWANGOSI YOU DIED SERVING THE NATION (Mwangosi umekufa ukilitumikia taifa)
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti katika kijiji cha Nyololo, Mufindi alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio na hata alipopiga kelele  za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa kikatili.

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA TUNAJIULIZA:-
Kwa nini askari polisi wamegeuka kuwa wauaji?
Nani amewatuma polisi kufanya mauaji?
Kwa nini wanafanya hivyo hawachukuliwi hatua?
Ni nani anayewafanya polisi wawe juu ya sheria?

Dakika moja ya ukimya kwa waandishi ....... ndani ya uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza

SOTE TUNALAANI!!!



Sikiliza Tamko la MPC kulaani mauaji ya mwandishi Mwangosi kwa kubofya play.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC) Deus Bugaywa akisoma 

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Kumbe mwanza tunawandishi wa habar weng hv,nilikua cjui hongera sana kwa kujitokeza kuungana na wenzenu kupinga kilichotokea!

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.