Leo ndio ile siku ambayo Gaidi aliyezalishwa na Wamarekani Osama
Bin Laden, aliwageukia na kuyalipua majengo pacha kule Marekani. Kwa waliokuwa wahanga wa matukio mbalimbali ya Kigaidi blogu hii
yawapa pole sana.
Wakati huo huo:- Tovuti rasmi ya serikali ya Yemen,
imesema kuwa naibu kamanda mkuu wa kundi la kigaidi la al qaeada katika rasi ya
Arabia ameuawa.
Tovuti hiyo imesema kuwa jeshi la nchi hiyo limemuua Said Ali
Al-shihri, raia wa Saudi Arabia ambaye aliachiliwa huru na Marekani kutoka
gereza la Guantanamo Bay mwaka wa 2007.
Hata hivyo kifo cha Al Shihri hakijathibitishwa.
Ripoti zinasema Al shihri ameuawa kusini mwa Yemen ambako
majeshi ya serikali yamekuwa yakipambana na wanamgambo wa Kiislamu kwa miezi
kadhaa sasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.