ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 21, 2012

WAZIRI MKUU MELES ZENAWI WA ETHIOPIA AMEFARIKI

Mara kadhaa hali yake iliripotiwa kuwa katika utata hali iliyosababisha wengi kukata tamaa juu ya hatma yake na haimaye sasa hatuko naye tena kiongozi huyo.
Alikuwa na umri wa miaka hamsini na saba na ni mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa na ambaye utawala wake ulikumbwa na utata barani afrika.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa sasa ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu alichokuwa akiugua hasa.

Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa akipokea matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa hospitali, ''Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo, alifariki jana mwendo wa 23:40,'' taarifa hiyo imesema.

Hayati Zenawi
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.

Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.

Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga ameiambia BBC kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles Zenawi.

Alisema kuwa hali nchini humo sio nzuri huku vita vya kikabila vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama kiongozi mashuhuri na mwenye elimu bora, aliyejitolea kuunganisha bara la afrika.
Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn anatarajiwa kuchukua mahala pake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.