ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 23, 2012

MCHUANO NI MKALI NAFASI ZA JUU CCM MWANZA DIALLO KUGOMBEA UENYEKITI CCM MKOA : NYAMAGANA USPIME NI SHILATU, NZUNGU NA KAGUNA!!

Antony Diallo akirudisha fomu ya Uenyekiti CCM Mkoa wa Mwanza kwa mpokeaji Zubeda Mbarouk ambaye ni katibu Sekretarieti na maadili mkoa wa Mwanza.

Kutokana na zoezi hilo kuanza kushika kasi kumeonyesha kuwa kazi ya kumpata mwenyekiti wa nafasi ya Mkoa kuonekana kuwa ngumu naya mikiki ya kila aina ya vijembe kwa wagombea wa nafasi hiyo kupishana katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza tangu kuanza kwa zoezi hilo.

Dkt.Athony Dialo ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Ilemela (CCM)kabla ya kushindwa na Highness Kiwia wa CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 amekuja na moto mkubwa akitishia shavu la mwenyekiti wa sasa anayetetea nafasi hiyo Bw.Clement Mabina (tangu mwaka 2007)



Msikilize Mh. Antony Diallo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mwanza, azungumzia mikakati yake, sababu za kugombea pia ajibu kuhusu kushindwa kwake Ubunge uchaguzi 2010. (Bofya play)

Raphael Shilatu akirudisha fomu ya kugombea Uenyekiti CCM Wilaya ya Nyamagana kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Deogratius Lutta.

Mashaka Kamchape Kaguna akirudisha fomu ya kugombea Uenyekiti CCM Wilaya ya Nyamagana kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Deogratius Lutta.

Emmanuel Nzungu akirudisha fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana  kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Deogratius Lutta.

Mashaka Kamchape Kaguna akishow love na Raphael Shilatu walipokutana nje ya chumba cha kurudisha fomu ndani ya ofisi za CCM Nyamagana wakati wa kurudisha fomu ya kugombea Uenyekiti CCM Wilaya Hiyo.


Sikiliza alichoongea Raphael Shilatu wakati akizungumza na Wandishi wa habari Mwanza. (Bofya play)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.