ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 19, 2012

FBME TAWI LA MWANZA WATOA MSAADA WA VYAKULA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA EID KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA KIISLAMU MISBAL HUUDAL

Meneja wa Benki ya FBME Tawi la Mwanza Joseph Gwalugano akimkabidhi mbuzi kijana Ally Shahban kwa niaba ya watoto wenzake kituo kulea watoto yatima cha MISBAL HUUDAL kwaajili ya chakula kituoni hapo hasa katika zama hizi zasikukuu.


Msikiti wa Al Aqswa uliamua kuanzisha kituo hiki kwa ajili ya kuweza kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu, wajane pamoja na watoto yatima ili kuiepusha jamii na kuwa na idadi kubwa ya watu kundi lisilokuwa na uelekeo.


Mfanyakazi wa Benki ya FBME tawi la Mwanza Anna Lupemba akiweka sawa msaada kwa kituo cha watoto yatima Mwanza.


Wadau wa kituo cha watoto yatima cha Misbal Huudal kilichopo mahina jijini Mwanza wakishusha zawadi ya Eid iliyotolewa na Benki ya FBME Tawi la Mwanza.


Vijana waliohudhuria makabidhiano hayo ya msaada kutoka benki ya FBME Tawi la Mwanza.


Wafanyakazi wa Benki ya FBME Tawi la Mwanza Joane Chovenye na Rose Mnyeke wakimkabidhi zawadi ya mbuzi mwalimu Rebeka Mgoni wa Shule hiyo ya watoto yatima kama sehemu ya msaada kwa kituohicho kusheherekea vyema sikukuu ya Eid El Fitri.


Meneja wa Benki ya FBME Tawi la Mwanza Joseph Gwalugano akimkabidhi mafuta ya kula maalim Mohamed Shahban  kwa niaba ya Uongozi wa walezi kituo kulea watoto yatima cha MISBAL HUUDAL kwaajili ya chakula kituoni hapo hasa katika zama hizi za sikukuu.


Neno la shukurani kutoka kwa Uongozi a kituo cha kulelea watoto yatima cha MISBAL HUUDAL kwa Benki ya FBME Tawi la Mwanza.


Imekuwa ni ada kwa benki ya FBME Tawi la Mwanza kila mwaka kutenga sehemu ya faida yake kusaidia watoto yatima naam na safari hii hilo limekamilishwa.
Hongereni FBME.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.