Mh. Ghalib Riyami akiwaasa jambo washiriki miss Utalii. |
Mh. Ghalib Riyami na picha ya pamoja na washiriki hao. |
MHESHIMIWA DIWANI ILALA ATEMBELEA KAMBI YA
MISS UTALII ILALA NA KINONDONI
Diwani wa kata ya mchikichini na mwenyekiti wa madiwani wa kata tano (ilala, mchikichini,
kariakoo,gerezani na jangwani) mheshimiwa Ghalib Riyami ametembelea kambi ya washiriki
wa Miss Utalii wilaya ya Ilala 2012 na Miss Utalii Wilaya ya Kinondoni2012
Kambi hiyo ya pamoja kati ya warembo wanao wania taji la Miss Utalii Ilala 2012
na wale wanao wania taji la Miss Utalii Kinondoni 2012 ipo katika Hoteli ya
kitalii ya Nyota 3 ya Lamada Hotel.
Mheshimiwa diwani ameelezea kufurahishwa kwake kwa wilaya
ya Ilala kupewa heshima ya kuwa wenyeji wa shindano hilo la kihistoria ambapo
wilaya mbili kwa pamoja zinashindana kuwania mataji ya wilaya zao katika ukumbi
na steji moja tena siku moja. “Najua waandaaji wangeweza kuamua shindano hili
lifanyikie kinondoni,lakini mmeamua kutupa heshima hiyo sisi wa wilaya ya ilala,hakika
tumefarijika sana” Aidha katika kuonyesha furaha yake na kupokea heshima hiyo
aliyo iita kubwa Mheshimiwa diwani aliahidi kuwa yeye binafsi pamoja na
madiwani wa wilaya ya ilala watahakikisha wanasaidia na kuunga mkono kwa hali
na mali kufanikisha kufanyika kwa shindano hilo,kama lilivyopangwa yaani tarehe
14/09/2012 katika hotel ya Lamada.
Aliwataka warembo wanaoshiriki shindano hilo kutambua
kuwa shindano hili tofauti na mashindano mengine ni alama ya urithi wa Taifa na
kielelezo cha utamaduni wa mtanzania,hivyo wanapaswa kutambua kuwa na nidhamu
na kuvaa uhalisia wa mtanzania siku zote na wakati wote mashindanoni nan je ya
mashindano.
Amewakumbusha na kuwaomba kutumia shindano hili kutangaza
utalii wa Wilaya ya ilala na mkoa kwa ujumla ikiwemo UWANJA WA NDEGE WA Juliasi
Nyerere,Soko la kariakoo,makumbusho ya taifa,sokola kimataifa la samaki la
magogoni,shule ya Pugu ambayo mwalimu Nyerere alifundisha, na ufukwe wa bahari
ya hindi.
Mheshimiwa diwani aliwashukuru na kuwapongeza wadhamini
mbalimbali ambao wamethibitisha kudhamini shindano hili,wakiwemo Lamada |hotel,105
Times FM Radio,Kahama Gold Mine,Traventine Hotel,Mzee Yusuph Enterprises,Easy
Media,Daja Saloon,Zizu Fashion,Tambaza Cort Brocker and Action Mart,Dagaa
Finance na Aucland Travel and Tours,Hameed Designer.Gabriel Designer Ametoa wito kwa makampuni na watu mbalimbali
kudhamini na kuchangia shindano hili ambalo gharama za kuandaa ni kubwa hivyo
kuhitaji mchango wa hali na mali.
Jumla ya warembo ishirini na nne(24)kumi mbili kutoka
wilaya ya kinondoni na kumi na mbili kutoka wilaya ya Ilala kwa pamoja
watachuana ili kupata taji la miss utalii wa wilaya ya Ilala na miss utalii wilaya ya kinondoni.Wilaya ya
Ilala washiriki ni; Zourha Malisa, Nancy Musheruzi, Princess Lemi, caroline
Yust, Eunice George, Naomi Michael, Lucy Julius, Nurina Mikindo, Rose James,
Salome Kiula, Marry Wambura na Judith Frank. Wahiriki wa
wilaya ya Kinondoni ni; Mwasiti Thabit, Irene Richard, Hellen Herman, Fatma Hussein,
Rachel Magai, Neema Mbeju, Neema Ngowi, Duda Tumbo, Zahra Waziri, Janeth Nelson, Teddy Paul na Ruby Kivunjo.
Akizungumza na warembo hao muheshimiwa diwani alisisita
umuhimu wa warembo hawa kulitumikia taifa kwa kutangaza vivutio vya kitalii
kitaifa na kimataifa ili kusaidia kuinua uchumi na kuongezeka kwa pato la taifa
wakati huu ambapo sekta ya utalii inachangia asilimia zaidi ya kumi na saba(17%)
ya pato la taifa.
Alisisitiza umuhimu wa kuelimisha vijana mashuleni ili
kukuza na kuhamasisha utalii wa ndani pia alisisitiza haja ya kutangaza kwa
nguvu zote vivutio vya utalii vya nchi yetu ya Tanzania ili kuongeza idadai ya
watalii wanaotembelea, ikiwa hadi leo kulingana na takwimu Tanzania hutembelewa
na watalii laki nane(800,000) kwa mwaka na hii ni idadi ndogo ukilinganisha na
nchi jirani zinazotuzunguka.
Pia alitoa wito kwa wazazi kuondokana na dhana potofu juu
ya mashindano ya urembo na aliwaasa mabinti kuwa na heshima, adabu na haiba
nzuri ili kuifanya jamii kubadili mtazamo juu ya mashindano haya yenye tija kwa
taifa letu kwa kuwa linatangaza utalii wa taifa hili la Tanzania.
Mwisho aliahidi ushirikiano wa hali na mali katika
kufanikisha shindano hili ambalo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa lamada hotel
ambao upo katika umoja wa kata tano anazoziongoza.
Yelemia Myenga
Mkurugenzi Miss Tourism Tanzania Organisation – Ilala na
Kinondoni
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.