ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 29, 2012

WALIMU WASHINIKIZA KUGOMA HAPO KESHO


Na Mwandishi wa Blogu hii
Shomari Binda,
Musoma


Chama cha walimu (CWT) Mkoa wa Mara kimewasihii walimu kutohadaika na kauli ya Serikali ya kuwataka kutogoma kwani haki zao bila kuchua hatua hiyo kamwe hazitatimizwa kwa wakati.

CWT imesema upatikanaji wa maslahi bora ya kazi yatapatikana kwa kushirikiana katika mgomo utakaoanza kesho ili Serikali ione umuhimu wa madai yao ambayo wamekuwa wakiyadai kwa muda mrefu sasa bila kupatiwa ufumbuzi.

Katibu wa CWT Mkoa wa Mara Fatuma Bakari amesema walimu wasiwe waoga kutetea haki zao kwani mgomo huo huko kisheria na kinachofanywa na Serikali ni vitisho kwao ambavyo amesema havina msingi.

Bakari amewakumbusha walimu kuwa madai yao ya maslahi bora ni ya muda mrefu huku akihituhumu Serikali kuendelea kuyapuuzia na kuwafanya kuishi maisha duni na kifukara licha ya kufanya kazi kubwa nayakujituma.

Uchunguzi uliofanywa na na mwandishi wa blogu hii Mjini Musoma umeonyesha kuwa mgomo huo hupo kesho na walimu wengi wamenukuliwa wakisema wako tayari kugoma ili kuishinikiza Serikali kutatua kero zao wanazozidai.

Walimu hao wamesema kamwe hawawezi kuwasaliti viongozi wao wa Kitaifa waliowachagua na kuwaachia vita hiyo ya madai ya msingi wapigane wenyewe kama vile wanapigania maslahi yao binafsi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.