ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 29, 2012

MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU SENSA YAMALIZIKA KWA MATOKEO YA KURIDHISHA JIJINI MWANZA, KILICHOBAKI TUJIANDAE KUHESABIWA

Afisa uhamasishaji Sensa Makao makuu Bw. Said J. K. Ameir
Bofya hapa juu kumsikiliza Afisa Mkuu Uhamasishaji Sensa Tanzania kupitia mahojiano aliyofanya na blogu hii mara baada ya mafunzo kumalizika leo hii jijini Mwanza.



Waandishi wa habari toka kanda ya ziwa, kati na magharibi wakiwa kwenye zoezi la vitendo kujifunza namna makarani wa Sensa wanavyofanya zoezi la uhesabu watu litakavyofanyika.


Awali zoezi la vitendo lilikuwa gumu kueleweka lakini kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele washiriki walikamata vilivyo na kufahamu vipengele husika.


Sensa yawatu na makazi itafanyika tarehe 26 Agosti 2012 ikiwa ni miaka kumi baada ya Sensa ya mwisho iliyofanyika mwaka 2002. Sensa nyingine zilifanyika katika miaka ya 1976, 1978 na 1988. Zoezi la kuhesabu watu katika Sensa hii litadumu kwa muda usiozidi siku saba.


Afisa Uhamasishaji Sensa Said Ameir akisaidia kutoa ufafanuzi kwa moja ya washiriki Abdallah Gankan ambaye ni Mwandishi wa habari toka Redio ya kiislamu jijini Mwanza, Iqra Fm.




Moja kati ya waelimishaji akitoa uelekezi kwenye mafunzo hayo ya vitendo yaliyofanyika kwa siku mbili na kumalizika leo katika ukumbi wa mikutano Annox Hotel jijini Mwanza. Sensa hii ina maswali yapatayo 62 yakihusisha maswali ya kilimo, Watanzania waishio nje ya nchi na mengineyo ikilinganishwa na Sensa ya mwaka 2002 ambayo ilikuwa na maswali 37. Lengo la maswali haya ni kukusanya takwimu zaidi ambazo zitatoa hali halisi ya Watanzania kidemografia, kiuchumi na kijamii.


Yapo maswali ya msingi ambayo huulizwa katika Sensa zote na maswali mapya kulingana na mahitaji ya kitakwimu ya sasa na miaka ijayo ambapo waandishi wa habari wamepewa nafasi hii ya mafunzo ili kupenyeza taarifa kuwaandaa wananchi.


Mkufunzi ambaye ni mwanasheria Ndg. O. Mangula akitoa elimu kuhusu Sheria za Sensa.


MUHIMU:- Inawezekana katika usiku wa kuamkia Sensa, mgeni alilala kwenye kaya na akaondoka kabla ya Karani wa Sensa hajafika. Kwa utaratibu wa Sensa mgeni huyo atatakiwa kuhesabiwa hapo alipolala na siyo huko atakapokutwa baada ya siku ya Sensa. Kwa ajili hiyo nivizuri kwa mkuu wa kaya akapata majibu ya maswali yote yatakayoulizwa kabla mgeni huyo hajaondoka ili aweze kuyajibu maswali ya Sensa kwa niaba ya mgeni wake. Karani wa Sensa atafika katika eneo la kuhesabia watu siku tatu kabla ya siku ya Sensa kulitambua eneo na kuwaandaa wakazi wa eneo hilo.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.