Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Amina Keita (kushoto) akitoa
zawadi ya simu kwa mmoja wa wakazi wa Mtwara, Nasra Salehe wakati wa
uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa mjini
Mtwara jana. Tukio hilo liliambatana na burudani kutoka kwa wasanii
chipukizi wa mkoani humo na baadhi ya wasanii maarufu kutoka katika Jiji
la Dar es Salaam ambako waliohudhuria walielezwa jinsi ya kujiunga na
faida mbalimbali zinazopatikana katika huduma ya Supa 5.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akihutubia wakati
akizindua huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani
Mtwara jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT, Mwansiti Almasi akikonga
nyoyo za wakazi wa Mtwara waliohudhuria uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya
Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akitoa zawadi ya
simu kwa Jamimu Mohamed baada ya kuibuka mshindi kwa kutoa maelezo
sahihi ya jinsi ya kujiunga na faida za huduma ya Supa 5 ya
Airtel wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana.
Airtel wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana.
Msanii mkali wa miondoko ya bongo flava, Juma Kassim Nature ‘Sir
Nature’ kutoka kundi la Wanaume Halisi, akifanya vitu vyake wakati wa
uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani
Mtwara jana.
Mwanamuziki wa miondoko ya hip hop, Ibrahim Mussa anayekwenda kwa jina
la ‘Roma Mkatoliki’ akighani moja ya shairi la wimbo wake uliompatia
umaarufu wa ‘Pastor’ katika uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel
katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Mtwara na viunga vyake wakifuatilia
uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa mjini
humo jana.
Mabinti wa Mtwara wakichuana ili kumpata mshindi wa kusakata ‘Kiduku’ ambapo mshindi wake, Nasra Salehe (kushoto) alijishindia simu katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel Mkoani Mtwara
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.