Siku ya kuzaliwa kwake pia inaadhimishwa na Umoja wa Mataifa kutokana na mchango wake katika kuikomboa Afrika Kusini dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Na nchini Afrika Kusini kwenyewe Nelson Mandela, ataadhimisha siku hii na
familia yake na Marafiki huku shughuli mbalimbali zikiandaliwa nchini humo kama
katika kusherehekea siku hii.
Mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini, Omar Murtasa, amesema kuwa Mzee Mandela anaheshimiwa na watu wengi nchini humo, wakitambua juhudi zake za kupigania Uhuru wa Taifa hilo lilolokuwa likiongozwa kirasmi na Ubaguzi wa rangi.
Ripoti zinasema raia wa nchi hiyo hii leo watajitolea kufanya kazi ya kuwasaidia wasiojiweza kwa muda wa dakika sitini na saba kama njia moja ya kuadhimisha siku hii.
Watoto kutoka shule ya msingi Batsogile mjini Soweto wakiimba wimbo husika kumtakia kheri Nelson Mandela, ambaye wao humwita either "Tata" (father) or "grandfather" kisha wakakata keki kwa heshima ya Mwanamapinduzi huyo wa Afrika.
Mandela aliachikiliwa huru kutoka gerezani akiwa na umri wa miaka 67.
Mandela alichaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini mwaka wa 1994.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.