ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 16, 2012

MADAWATI 1000 YAFANYIWA MRADI WA TASAF HILO LAGUNDULIKA BAADA YA MH MKONO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHULE YA SEKONDARI BUTUGURI

Madawati zaidi ya 1000 yaliyotengenezwa na Mfuko waMaendeleoya Jamii TASAF, kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Butuguri iliyopo katika Halmshauri ya Musoma mkoani Mara yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi shuleni hapo.


Akiongea na waandishi wa habari Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono alisema kuwa kumekuwepo na wizi mkubwa katika miradi mbalimbali ya TASAF hivyo hayuko tayari kuona wizi huo unaendelea katika jimbo hilo

Alisemamiradi iliyotengenezwa na Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii haifai ikilinganishwa na shule hiyo ya Butuguri aliyoijenga kwa fedha zake,huku wezi wa fedha za mfuko huo wakiendelea kulindwa
Mh Mkono amesema kuwa kumekuwepo na desturi ya kumkamata mwizi wa kuku na kumua lakini watu wanaoiba na kutumia fedha za Umma vibaya wakiachwa bila kukamatwa.

Mbunge huyo akionyesha kukasirika kutokana na ubadhilifu huo wa fedha za Madawati hayo alisema atabeba madawati hayo na kuyarudisha katika halmashauri hiyo na yeye kuleta madawati mengine kwa matumizi shuleni hapo. 
 Aidha madiwani kutoka Halmashauri hiyo Luti Mayamba na Thomas Nyasiro waliokuwa wameambatana na Mbunge huyo wamesema vitendo hivyo si vya kiungwana kwani inaonyesha dhahiri viongozi wanavyotumia madaraka yao vibaya na kuahidi kufika suala hilo katika baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe.
Madawati hayo zaidi ya 1000 yaliyotengenzwa na MfuKo wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa zaidi ya shilingi milioni 50 chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashuri hiyo Dr Karnai Kunei yameharibika muda mfupi mara baada ya kuanza kutumika.

Mh. Nimrod Mkono (kulia) akiwa na mwandishi wa habari wa ITV George Mataro pindi alipofanya ziara ya kushtukiza katika shule ya sekondari Butuguri iliyopo katika Halmshauri ya Musoma mkoani Mara .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.