ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 16, 2012

EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 YAMALIZIKA KWA WAWILI TU... KUTWALIWA TOKA MWANZA

Mwanza itawakilishwa na washiriki wawili tu katika mchakato wa kitaifa kutafuta washiriki watakaoingia kwenye kambi ya EBSS jijini Dar es salaam pichani ni majaji wa EBSS mwaka 2012 Master J, na Salama Jabir wakimkumbatia Madam Ritha (katikati) mara baada ya shughuli nzito kumalizika jana katika ukumbi maalum uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Madam Ritha akishow Love na Jamaa aliyeweka rekodi.... Bubu aliyejitokeza kwenye shindano na kushindana kuimba (search BUBU AFANYA KWELI EBSS MWANZA)

Kijana mdogo kuliko wote ambaye kama vigezo vya kubanwa na shule visingekuwepo na kwasababu EBSS inathamini Elimu, basi alikuwa na ushawishi mkubwa kwa majaji. 

Akifanya mahojiano mara baada ya kutoka chumba cha usaili.

Mmechisho umo-mo.

Washiriki walipata vinywaji bure toka Coca cola.


Waliochemsha walipataje shida kuzing'oa namba zao...

Full kujiamini... mstarini kuelekea usailini..

Thats wozup...


Pamoja na kwamba mwaka huu mkoa wa Mwanza umeongoza kuwa na idadi kubwa ya vijana waliojitokeza kushiriki EBSS lakini haikuweza kutoa washiriki wenye uwiano sahihi na waliojitokeza hivyo kupigwa bao na mikoa mingine iliyokuwa na washiriki wachache lakini walifaulu ni watano na kuendelea. 

Kutoka Mwanza hadi Dar es salaam ni umbali wa kilimeta 1200 na  ni washiriki 1200 waliojitokeza kwenye usaili wa EBSS Mwanza, kati ya hao ni 8 tu ndiyo walionekana kuwa na vipaji toka moyoni inamaana kuwa utatembea wastani wa  kilometa 150 ili kumpata mshiriki mmoja hadi mwingine,  na hatimaye wawili tu kati ya hao nane wakapatikana na sifa husika na kuteuliwa kuwakilisha jiji la Mwanza kwenye kinyang'anyiro kikuu Bongo Dar es salaam.  
Jeh Mwanza haina vipaji now days?


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.