ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 15, 2012

MASWALI MENGI YAZUKA MARA BAADA YA TAARIFA ZA ANAYEDAIWA KUMTEKA Dk ULIMBOKA KUKAMATWA




Kwa msaada wa jukwaa lenye kuzua changamoto nyingi katika masuala mbalimbali, jukwaa ambalo kwa sasa limekuwa chanzo cha habari muhimu nchini Tanzania na dunia kwa ujumla nalizungumzia Jukwaa la Wanamabadiliko, G.Sengo Blog imepata maswali mengi humo ambayo kimsingi natumaini nawe yatakujenga... Chekshia wadau walivyo tiririka...

Jones Nyakwana
Tunasubiri huyo mtumishi wa Serikali aliyewakodi. Pia tujue hiyo Nyumba waliyompeleka kabla ya kumfikisha msituni. Pia waseme dereva wa hiyo gari alikuwa ni nani maana kamwe siyo Mkenya. Lakini tukumbuke kila uongo una mwisho.
Mouddy Mtoi
Nimeyapenda sana haya maswali kutoka kwa jamaa yangu mmoja pale jf. Mimi nimejiuliza mkenya a riot squad gangster ndani ya tz aliingiaje? aliwezaje kuendesha gari isiyo na plate namba? Cha ajabu kabisa alipajuaje mabwepande ambapo hata sisi tuliopo Dar es salaam wengine hatupajui?
Majibu niliyopata ni mzoefu wa kuplot assassination ndio maana akawa trusted.
Swali jingine likazuka why did he fail this time? Nikapata jibu ni bahati mbaya tu. Nika conclude waliomtuma hawakuwa na uhakika na kazi yao walikuwa wanabahatisha tu. Hapo na penyewe pakazuka maswali a riot squad gangster fail or not angebaki tanzania? What was he doing? And where was he hiding? And why going for confession? And waliomtuma kwanini hawakumrudisha walikomtoa iwe alifaulu ama alifeli? Na kubwa kuliko yote hivi utamuajiri assassin expert from near by country halafu aje afail kweli? Manake to me ni lazima awe serial killer mzuri and well experienced in that field vinginevyo ni hatari sana kwako. Mtanisamehe tu dont read my mind here.
Katulanda na \Mtoi,
Jamani walau mpeni hogera Kamanda Kova kwa kuwalisha stori hii waandishi wa habari wa Tanzania kufanikiwa kutoka na front page ya magazeti karibu yote BILA KUAMBATANA NA PICHA ya huyo mtekaji mkristo mlokole anayetubu kabla ya kulipwa baada ya kazi...Inabidi tuseme kuna wasanii wengi nchi hii jamani...

Mwl. Lwaitama,
Mimi nina wazo, kwamba badala ya kuhangaika na madini, gesi asilia, mafuta ya uchuro wa muungano, kilimo kwanza, viwanda njaa, utalii na usumbufu mwingine tusiouweza, ni heri sisi wote kabisa, kama taifa, tukajikita kwenye biashara ya kutengeneza filamu kwa ni tuna hazina kubwa ya wakurugenzi/waelekezaji na waigizaji.

Ahahah!! Ila nadhani jamaa zetu wa wana habari tusaidieni tupate picha ya huyu mbaya wetu kutoka Kenya kusudi sinema hii izidi kunoga!!! Hivi ni kweli eti Kanisa alikodaiwa kwenda kutubu huyu jamaa hata kabla hajalipwa limekana kuhusika....??? Maana ulokole wake kanisa utaingia doa kama kumbe walikole wake ni watezaji kutoka nchi jiarani....Ahaha!!! Ngoja tusije tukawaudhi sana jamaa wasanii hawa wakatutumia mmoja wa wale 11 ambao bado sijui nao wapo nchini wanagoja heal zao au wao walipata na wameisha ondoka...Ahah!!! Nchi hii bwana!!!

Richard Mgamba,

Kaka yangu Matinyi, Umenifanya nikacheka mpaka nikamwaga divai yangu leo jumapili, na ninaendelea kucheka kila nikisoma ulichoandika mbavu sina. Nadhani tutauza sana kuanzia filamu ya mapanki, Ulimboka, Mjengoni, na madudu mengi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.