ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 8, 2012

MANCHESTER CITY WAIBUKA KUWA MABINGWA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA MWANZA

Timu ya soka ya mashabiki wa Manchester City imeibuka kuwa mabingwa wa Serengeti Fiesta Soka bonanza kwa jiji la Mwanza lililofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana, mara baada ya ushindi wa penati dhidi ya Real Madrid ambao walikuwa wakitetea ubingwa wao waloutwaa mwaka janakwenye mashindano hayo.

Msimamizi mkuu wa Bonanza la Serengeti Fiesta Soka Bonanza jijini Mwanza John Tegete akitoa maelezo ya sheria za zitakazo endesha mashindano hayo.
Kikosi cha timu ya mashabiki wa Barcelona kilichoshindwa kuingia nusu fainali kwa kuzidiwa magoli na Chelsea kundi A.

Washindi wa pili Real Madrid waliozawadiwa kitita cha shilingi 200,000/= na kreti moja ya Serengeti Lager.

Timu ya Alsenal iliyoingia nusu fainali na kutolewa na Man City.

Kikosi cha Chelsea kilichoishia nusu fainali mara baada ya kukandamizwa na Real Madrid.

Kwa mara nyingine Manchester United hawakuweza kuwa tishio kwa mashindano hayo ingawa mwaka huu timu hiyo wameonyesha kuimarika.

Kikosi cha Baryen Munich ambacho safari hii kimeonyesha uhai zaidi.

Liverpool mwaka huu kwa jiji la Mwanza imeshindwa kuonyesha makali na msisimko wa aina yoyote licha ya kikosi chake kusheheni vijana wengi wadogo.

Mashabiki waliojinafasi jukwaa kuu kushuhudia Serengeti Fiesta Soka bonanza iliyofanyika leo kuanzia majira ya saa mbili asubuhi kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Dadaz wa kutoa huduma ya vinywaji viwanjani humo.

Vigezo na masharti kwa mashabiki vilizingatiwa kwa mashabiki kunyuka nyuzi za timu zao.

Benchi la waamuzi wa Bonanza hilo.

Clouds Tv Sports Bar mzigo mzima kuruka pale.

Rais wa washindi wa pili Real Madrid akipokea 'umateumate' aka 'chapaa' kiasi cha shilingi laki mbili taslimu toka kwa mratibu wa Serengeti Fiesta Soka Bonanza kituo cha Mwanza, Shaffi Dauda.

Rais wa washindi Manchester City akipokea 'umateumate' zawadi kwa timu yake kiasi cha shilingi laki tano taslimu toka kwa mratibu wa Serengeti Fiesta Soka Bonanza kituo cha Mwanza, Shaffi Dauda.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.