Anaitwa Yvona Kamugisha (10) binti wa Julius Kamugisha (32) ambaye ni mkazi wa Kirumba wilaya ya Ilemela jijini Mwanza anaomba msaada wa fedha toka kwa wasamalia wema kote nchini kwaajili ya nauli na chakula ili apelekwe KCMC mkoani Kilimanjaro kwaajili ya matibabu zaidi ya moyo.
Vithibitisho vya madaktari. |
Mwaka 2008 baada ya kupelekwa Hospitali ya KCMC- Moshi mkoani Kilimanjaro na kugundulika kuwa na tatizo la kupanuka kwa Moyo wake alifanyiwa operesheni kisha kuruhusiwa baada ya matibabu.
Mtoto Yvona amerudiwa na Tatizo hilo baada ya kupata vipimo vya wataalamu toka nchini India waliofika nchini katika Hospitali ya Hindu iliyopo mtaa wa Nyakahoja barabara ya Balewa jijini Mwanza walio baini kujirudia tatizo hilo.
Kwa yeyote atakaye guswa tafadhali awasiliane na baba wa mtoto katika nambari zifuatazo 0754 724278 au 0782 946177 kwa ajili ya kuwasilisha mchango wako.
Aksanteni wadau.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.