Mwenyekiti wa Ziara hiyo ya John Peter Kadutu amesema kuwa Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara,
timu ya Simba ya Dar es salaam watakuwa na ziara ya mechi mbili za kujipima nguvu na
pia kulitembeza Kombe la Ubingwa wa msimu huu katika mikoa ya Kanda ya
Ziwa.
Ziara hiyo ya Simba itafanyika miji ya Mwanza na Shinyanga ambapo wapenzi wa soka wa Kanda ya Ziwa watapata fursa ya kushuhudia mechi za timu hiyo, Kombe la Ubingwa ambalo litatembezwa kwenye mitaa mbalimbali jijini Mwanza mara baada ya timu hiyo kutua kesho jijini hapa kwa kutumia usafiri wa anga pamoja na kikosi kipya cha timu hiyo kwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara, Kombe la Kagame na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika ziara hiyo ya Simba, timu mbili zimealikwa ambazo ni Toto African ya Mwanza iliyopo ligi kuu soka Tanzania Bara na Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda The Express ya mjini Kampala ambapo zote hizo zitacheza na Wekundu hao wa Msimbazi.
Kwamujibu wa Katibu mkuu wa Chama cha soka mkoani Mwanza, Mabrouk amesema kuwa mechi ya kwanza itachezwa siku ya jumamosi ya tarehe 23/06/2012 katika dimba la CCM Kirumba ambapo itakuwa kati ya Simba na Toto Afrika ya Mwanza.
Mchezo ambao pia utakuwa ni sehemu ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Sherehe za wiki ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambayo kitaifa itafanyika jijini Mwanza.
Pia mchezo huo utatumika kuwatambulisha wachezaji wapya kwa timu zote mbili waliosajiliwa kwaajili ya msimu ujao na michezo mbalimbali ya kimataifa.
"Toto ni kama Chuo kila mwaka inasajili vipaji vya ukweli vyenye kumudu kombinesheni, timu imekwishaanza mazoezi ikiwa ni timu inayofanya usajili wa kawaida lakini ambao huvisumbua vilabu vikubwa Simba na Yanga ikiamini usajili si kusajili wachezaji kwa milioni 30 bali ni kusajili vipaji" asema Swalehe Akida kaimu katibu mwenezi wa Toto Africans.
"Tulipo mfunga Yanga bao 5-0 yalisemwa mengi ila cha msingi nawaomba watu waje washuhudie mpira wa kisasa kwamba tulibahatisha au laa, Simba na Toto zinapokutana mziki wake unajulikana mashabiki waje hiyo jumamosi CCM Kirumba kuona jinsi Simba inavyotoa kipigo cha aibu kwa Toto Africans" Mwenyekiti wa Simba kanda ya ziwa Ommary Makoye na tambo zake.
Jumapili ya tarehe 24/06 Simba itasafiri hadi mjini Shinyanga kukiputa na Express toka Kampala nchini Uganda mchezo utakao chezwa kwenye dimba la Kambarage.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.