ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 12, 2012

DUDU BAYA na MADUDU yake MPAKA HOME

Msanii long time kwenye game katika ya muziki wa kizazi kipya nchini, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya ameendeleza madudu yake kwa kuirejea tabia yake ya kuwadunda watu kijingajinga baada ya hivi karibuni (ilikuwa ijumaa) kumpiga mtangazaji mtulivu asiye na tabia za ukorofi kutoka kituo cha radio cha Kiss Fm, Ezden Jumanne aka The Rocker.
Dudu Baya.

Inshu ilikuwaje:
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kinasimulia  kuwa Ezden 'The Rocker' alikuwa ameandaa Onyesho lililokuwa lifanyike siku inayofuata yaani jumamosi lililoitwa Mwanza Blast ambapo msanii Dudu Baya ambaye kwa sasa anaishi jijini Mwanza alianza kuiponda show hiyo hali iliyosababishwa na kutopewa shavu la kutumbuiza kwenye consert hilo licha ya kuomba kushiriki, jambo ambalo linaonekana wazi kuwa lilimuuma.

Wakiwa katika Eneo la kona ya Bwiru karibu na MS Hotel wakitokea Nyakato National ambako Ezden na kamati yake walikuwa kwenye kikao kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusambaza kibali cha show kwa wadau husika, Dudu Baya alimfuata kibabe mtangazaji huyo na kuanza kumporomoshea matusi machafu ya nguoni kitendo ambacho Ezden hakukivumilia naye kuanza kujibu mapigo.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale Dudu Baya alipo semezwa neno ambalo lilionekana wazi kumaanisha ukweli uliopo kwa yeye katika sanaa ya muziki hali iliyopelekea kumaindi dizain, akachomoka kwa hasira toka kwenye gari aina ya Noah akamsogelea karibu na kumchapa kwa nguvu kibao cha usoni mtangazaji huyo.
Ezden 'The Rocker'



Kuona hali hiyo mtangazaji mwingine aliyekuwa ameambatana na Ezden, Philbert Kabago wa Passion FM akampa usaidizi mwenzie kwa kumfurumishia mangumi na mateke Dudu Baya hali iliyosababisha watu kujaa eneo hilo na hata wengine kutaka kumvamia Dudu kwa kuonyesha kukerwa na tabia hiyo ya ukorifi.


Dudu anasemaje?
Jana Clouds Fm kupitia kipindi cha XXL wamemhoji msanii huyo ambaye amesema sababu za kumpiga mtangazaji huyo ni kuwa alipofika Mwanza kwa mara ya kwanza aliitisha kikao cha wasanii wote wa jiji hilo ili kupanga mikakati ya kukuza muziki.   Kutokana na kikao hicho, Dudu anasema walianzisha chama walichokipa jina la ‘Mwanza Kwanza.’ Anasema miezi kama mitatu iliyopita alifariki rapper wa Mwanza aliyekuwa anaitwa Mo Chella kwa kuchomwa na kisu na ndipo Ezden aliandaa show ya kuchangisha fedha za kuisaidia familia ya marehemu bila kumshirikisha Dudu Baya.   Kutokana na kitendo hicho uhusiano kati yake na Ezden uliingia kasoro kiasi cha kutozungumza vizuri kila wanapokutana na ndio maana hivi karibuni alifikia hatua ya kumpiga.

Ukweli
Ni kwamba hajui imeanzishwa lini, hafahamu nia na malengo ya kuanzisha Mwanza Kwanza, Hajawahi kushiriki vikao vya Mwanza kwanza hata kimoja zaidi ya kuwa mstari wa mbele kuuvuruga umoja huo kwani hata wasanii kama H. Baba na Jully Tax pindi walipo onyesha ushirikiano na wasanii wa nyumbani (Mwanza) na hata kujiunga na umoja huo walipata meseji za matusi (ushahidi upo).

Kuhusu msiba wa Mo-Chella blogu hii ilikuwa shahidi hatua kwa hatua juu ya viongozi wa umoja huo walivyoshiriki kikamilifu kufanikisha uchangishaji fedha kupitia Show hadi hatua za mwisho zilipokabidhishwa kwa mama wa marehemu... ( KUISOMA BARUA YA MAMA WA MAREHEMU AKISHUKURU JITIHADA/MCHANGO WA WANA MWANZA KWANZA BOFYA HAPA  http://gsengo.blogspot.com/2012/04/barua-ya-shukurani-kwa-wana.html )

Kama tujuavyo kwa jadi ya mila na desturi za Afrika 'msiba hauna kadi' Sasa Pamoja na kupata taarifa za msiba wa msanii anayechipukia Mwanza, Dudu Baya hakuonyesha ushirikiano zaidi ya kusisitiza wimbo wake Pokopoko kupata air time kwa baadhi ya vituo vya radio Mwanza ile hali vituo hivyo vipindi vyake vingi vilikuwa kwenye maombolezo vikipiga nyimbo kufariji.

Blogu hii (G Sengo) inalaani kitendo hicho ambacho si cha uungwana kilichofanywa na Dudu Baya kwani hakina malengo mazuri na wasanii wa Mwanza pamoja na mziki wetu nchini kwa ujumla.

Tupe maoni yako

5 comments:

  1. mpumbavu huyo dudu baya, ubabe wake wa kifala aupeleke huko uswahilini kwao, kafulia kimuziki hana wimbo hata mmoja unaoweza kupigika katika show iwe ya studio ama ya kitaa zaidi amuangukie Fred Fidelis "Fredwaa" anayempa shavu, hana jipya mpuuzi tu huyo, shenzi typ, anampiga mchizi kifalafala, hata nami ningekuwa karibu ningembonda mjinga huyo

    ReplyDelete
  2. Mwambie co gemu wanasiasa wapgane na wasanii pia?? Ni sawa na mwanakamati anachangia laki then siku ya sherehe unagombania bia ya 2000, aibu atuachie mwz ndooshida

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa cjui niaje...lazima atakuwa choko hajaguswa kitambo anachokoza marijali wambashie,Falaa tu huyoo hajaenda shule na kakwama kimaisha kakosa wa kumlilia.I hate u Biiiiitch

    ReplyDelete
  4. Shenzi typ! achunge sana! huu ni muziki nasio masumbwi jeuri yake iishie kwao asidhani kila mtu wakupigwa pgwa fara kabisa kwa mwanza ameuwasha moto atapahama mpumbavu sana!.

    ReplyDelete
  5. NAHIYAJI BAUNSA AISEEEEE

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.