Chama hicho kinacho tegemea kufanya uchaguzi wake mkuu mnamo tarehe 23 juni 2012 tayari kimeanzisha utaratibu wa kutoa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi katika ofisi ya Afisa Utamaduni Michezo jiji la Mwanza tangu tarehe 7/06/2012 kwa ada ya shilingi 10,000/=, Tarehe ya kurudisha fomu imebainishwa kuwa ni 21/06/2012 saa 9:30 Alasili.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama cha mbio za Mitumbwi Mwanza Richard Mgabo amesema kuwa nafasi zinazo gombewa ni pamoja na
Nafasi ya Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti,
Katibu mkuu,
katibu mkuu msaidizi,
Mweka hazina,
Mweke hazina msaidizi,
Katibu mwenezi,
Mjumbe mmoja wa mkutano mkuu wa mkoa,
na Wajumbe wawili wa kamati tendaji.
Sababu kubwa za kuanzishwa mchezo huo ni kuwapa fursa wavuvi na wananchi kwa ujumla wao wanaoishi kandokando mwa ziwa Victoria ili waweze kushiriki mchezo huo wa mbio za mitumbwi baada ya shughuli zao za uvuvi pamoja na kukuza Utalii ndani ya Ziwa Victoria, kujipatia kipato cha kukuza mitaji kwa wale watakaoshiriki wakati wa mashindano na kushinda.
Awali mchezo huo ulionekana kama burudani tu lakini kwa sasa mbioza mitumbwi zimekuwa na unamvuto kwa watu wa mataifa mbalimbali na umeendelea kujipatia umaarufu ndani na nje ya Tanzania.
Mpaka sasa Kampuni ya Bia Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia ya Balimi ndiyo wadhamini wakuu wa mashindano ya mbio za mitumbwi kanda ya ziwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.