ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 30, 2012

WASAMARIA WEMA TWAOMBWA KUMNUSURU MTOTO HUYU MWENYE MATUNDU MATATU KWENYE MOYO

Video ya Neema.
Pichani mtoto Neema George aliyegundulika kuwa na matundu matatu kwenye moyo. 
Mtoto Neema George (16) amewaomba wasamaria wema wajitokeze kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.
Miguu ya Neema
Hali ya Neema George inazidi kuzorota siku baada ya siku, miguu ikiwa imevimba, akitaabika katika suala la kula, kuongea na akipata maumivu makali ya tumbo hasa nyakati za usiku.
Baba mzazi wa Neema, George Mugunga (kushoto) anasema kuwa mnamo mwaka 2010 mara baada ya hali ya mtoto wake kuzorota alimfikisha katika hospitali ya Rufaa Bugando kwaajili ya matibabu, lakini mara baada ya vipimo kufanyika vikaonyesha kuwa moyo wa mtoto wake una matundu matatu.
Baadhi ya vithibitisho vya tiba.
Madaktari kupitia kliniki aliyokuwa akipata huduma (Bugando) wamesema kuwa tatizo la neema ni kubwa na haliwezi kupatiwa ufumbuzi hapa nchini bali linaweza kupata tiba Nchini India kwa makadirio ya gharama ya shilingi za kitanzania milioni 25.

Picha za ukutani wakati wa ubatizo wa Neema, katika kipindi hicho ingawa hali yake ilikuwa dhoofu lakini suala la kuvimba tumbo na miguu halikuwepo.
Mbali na kumtegemea mungu kwa kila azungumzalo mtoto huyu anaonekana anaakili sana na mwenye uchangamfu wa ndani tatizo linabaki kuwa anaumwa.
Neema akiwa na mwandishi wa habari hizi Albert G. Sengo aliyefika nyumbani kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza kwaajili ya kuchukuwa taarifa zaidi.
Kutokana na kiwango kilichotamkwa kuwa kinahitajika kwa ajili ya tiba nje ya nchi, familia ya mtoto huyu ilikata tamaa  kabisa na kukata shauri la kumpeleka Sengerema kijijini ili akatibiwe na waganga wa kienyeji ndipo bwana Azizi Bukene (ambaye ni jirani yao) akashauri kuita vyombo vya habari kwaajili ya kulifikisha kwa umma kwa msaada.
Nje ya nyumba.

Video
Familia ya mtoto huyu inategemea kilimo kama sehemu ya kipato cha kuendesha maisha ya kila siku, hivyo uwezo wa kufikisha kiwango hicho cha fedha hata kupata matibabu kwa manufaa ya mtoto huyo kuendelee na masomo ni ndoto za alinacha.

Video
Baba wa mtoto huyo aitwaye George Lenatus Mugunga amewaomba wasamaria wema, makampuni, wanasiasa, viongozi wa dini, wafanyabiashara na watu binafsi walioguswa na tatizo la mtoto Neema, kuwasiliana naye kupitia namba za simu ya kiganjani 0755424086 au kufika Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza ili kupata utaratibu wa kufikisha msaada huo haraka iwezekanavyo.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Excellent beat ! I would like to apprentice while you amend your website,
    how can i subscribe for a blog web site? The account aided me a acceptable deal.
    I had been a little bit acquainted of this your broadcast provided bright clear idea
    My site > Games New

    ReplyDelete
  2. Great blog here! Also your site loads up very fast! What host are you using?
    Can I get your affiliate link to your host? I wish my web
    site loaded up as quickly as yours lol
    Also see my website - Games New

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.