Mheshimiwa Vick Kamata akikaribishwa kwa furaha na wanakijiji wa Bukoli na nyimbo za nyumbani zikitawala.
Hizi ndizo baiskeli walizokabidhiwa ndugu zetu wenye ulemavu kijiji cha Bukoli.
Pichani diwani viti maalum kata ya bukoli akimkaribisha mheshiwa Vicky Kamata kuongea na wananchi ambapo kwa upande wake alisema kuwa akinamama wenzake wa kijiji hicho wako mstari wa mbele katika majukumu mbalimbali kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Akinamama wa kijiji cha Bukoli waliowasindikiza ndugu zao ambao ni walemavu kupatiwa baiskeli wakisiliza yanayojiri kwa umakini juu ya utunzaji wa viwezeshaji hivyo vya usafiri kurahisisha shughuli za maendeleo.
Mh Vicky Kamata akiongea na wananchi wa Bukoli.
Wakisubiri kuwezeshwa na mradi wa Victoria Foundation.
Mpango huo wa ugawaji baiskeli kwa walemavu wa miguu haukuwanufaisha watu wakubwa pekee bali hata watoto.
Mh vicky kamata akimsaidia mmoja kati ya walemavu waliokabidhiwa baiskeli, kuvaa tshirt ya Victoria Foundation
Kijiji cha Bukoli.
Baada ya safari ndefu wadau wa Victoria Foundation walirejea jijini Mwanza kusaka mahitaji mengine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.