ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 3, 2012

MKESHA WA KUSIFU NA KUABUDU NA MAMBO YA TANZANIA NA AFRIKA KUFANYIKA MAY 4, 2012

Wachungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jiji Dar es Salaam (kutoka kushoto) Abel Orgenes na Paul Safari wakiwa na muimbaji wa nyimbo za injili John Lisu wakioongea na waandishi wa habari juu ya mkesha mkubwa wa uimbaji wa kusifu na kuabudu pamoja na maombi kwa ajili ya Tanzania na Bara la Afrika ujulikanao kwa jina la (AFLEWO) ambao unatarajiwa kufanyika 4 May, 2012 ndani ya kanisa la City Christian Centre (CCC)- Upanga jijini Dar es Salaam.

Mchungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jijini Dar es Salaam Paul Safari (katika) alisema kuwa mkesha kama huwa unafanyika pia katika nchi nyingi za Afrika, kama vile Kenya, Rwanda. Kauli Mbiu ya mwaka 2012 ni kutoka zaburi ya 68:1 'Lets God Arise'. Mkesha huu unaundwa na waimbaji zaidi ya 50 kwa kutengeneza timu moja yaani "Praise Team" na hakutakuwa na waimbaji binafsi.

Mchungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jiji Dar es Salaam Abel (katikati) akionyesha kauli mbiu ya mkesha huo ambao unasema, 'Lets God Arise'. Pembeni yake anayeshuhudia ni mchungaji Paul Safari (kulia) na Samuel Mwangati (kulia) ambaye ni Music Director wa Aflewo.

Kwa upande wake Samuel Mwangati ambaye ni Music Director wa Aflewo alisema kuwa madhumuni ya Mkesha huu ni kama ifuatavyo.
1. Kuwaungaisha Wakristo Kutoka madhehebu yote katika Kusifu na Kuabudu.

2. Kuwaleta Pamoja wakrtisto Kuomba kwa ajili ya Kuliombea Taifa la Tanzania na Bara la Africa kwa ujumla.

3. Kuleta Umoja wa Mwili wa Kristo. Pia aliongeza kuwa kamati ya maandalizi imeandaa utaratibu wa mabasi kuanzia Akiba, Palm Beach na Muhimbili ambapo yatafanya kazi kuanzia saa 1-3 usiku.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.