ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 3, 2012

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YATOA ELIMU YA MAZINGIRA KWA MAFUNDI MCHUNDO MWANZA

Mgeni rasmi bw. Ndaro Kulwijila ambaye ni Katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Mwanza akifungua warsha hiyo akisema: Uelewa mdogo wa wafanyabiashara wanaoingiza vifaa hasa majokofu na viyoyozi, kutozingatia kanuni za usimamizi wa mazingira sanjari na ongezeko la mafundi vishoka wanaotumia njia zisizo salama kwa afya na mazingira ni moja ya vyanzo vinazotengeneza kemikali haribifu zinazonomng'onyoa tabaka la hewa ozoni hali inayosababisha kuongezeka kwa ukali wa jua hivyo kusababisha ukame na teketezo la uoto asili, wanyama samaki na mimea.

Washiriki waliohudhuria ufunguzi huo wa mafunzo ya siku mbili kuhusu njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi na umuhimu wa sekta ya majokofu na viyoyozi kwa tabaka la hewa ya ozoni yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais nchini.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais, Magdalena John Mtenga amesema kuwa: Lengo la warsha hiyo ni kuongeza uelewa kwa wadau hao juu ya umuhimu wa kulinda tabaka la ozoni kwa kutumia njia salama za kuhumia majokofu na viyoyozi na kemikali/bidhaa mbadala rafiki kwa Tabaka la ozoni.

Zana za kufundishia...

Pia washiriki watapata fursa ya kuelimishwa kuhusu masuala muhimu ya nayolenga hifadhi ya tabaka la ozoni ikiwa ni pamoja na sayansi ya tabaka la ozoni na umuhimu wake, sheria ya usimamizi wa mazingira, huduma bora na salama ya majokofu na viyoyozi pamoja na teknolojia mbadala ya majokofu na viyoyozi.

Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha hiyo ya mafunzo kwa Mafundi Mchundo wa majokofu na viyoyozi na umuhimu wa sekta ya majokofu na viyoyozi kwa tabaka la hewa ozoni leo Hoteli La Kairo jijini Mwanza

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.