ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 16, 2012

WASEMAVYO WADAU JUU YA BREAKING NYUZ YA MWENYEKITI WA UVCCM ALIYEHAMIA CHADEMA

James Ole Millya (Mwenyekiti wa UVCCM Arusha) ajivua gamba na kuhamia CHADEMA
Source radio 5 arusha! Anaongea kwa hasira sana akisema CCM siyo baba wala mama yake! Anadai chama kinatumia fedha za walipa kodi kuzunguka nchi nzima kumchafua.Millya ambaye ni mfuasi mkuu wa Edward Lowassa, anaelezwa kutaka kupata nafasi ya kuwania ubunge Arusha mjini, lakini Chadema wamemkatalia, kama walivyomkatalia Lowassa, kwa maelezo kwamba bado si wasafi kubeba bendera ya chama chenye nia ya kupambana na ufisadi. Chadema wanawakaribisha wote kwa sharti la kuwa wanachama wa kawaida, na watapewa muda wa kujisafisha na kuwaomba radhi Watanzania.

KAULI ZA WADAU:-
@ Wana Mabadiliko,Chukueni mfano rahisi sana! Kama mtu alikuwa jambazi, muuaji kitendo cha yeye kubadili mtindo wa maisha yake na kuingia kanisani na kujiita mkristo mpya, moja kwa moja anakuwa ametakaswa dhambi zake. Katika siasa kwa sasa hapa Tanzania CCM na CHADEMA ni vyama vinavyosimama kwenye grounds tofauti kabisa za kisiasa. CCM inasimama upande wa ufisadi na uongozi mbovu ulioshindwa kuwatumikia wananchi wakati CHADEMA inasimama upande wa wapinga ufisadi, upande uliojitoa kuwatumikia wananchi na kuwapa sauti na kupigana dhidi ya utawala mbovu wa nchi hii. Kitendo cha Millya kucross over na kuingia CHADEMA kinamtakasa kama mpagani niliyemwelezea hapo juu anavyotakaswa na kitendo chake cha kuingia na kubatizwa kujiunga na kanisa.Karibu CHADEMA Ole Millya, karibu mahali tunakowatumikia wananchi badala ya matumbo yetu!Maingu Samson Mwigamba,Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha.

@Pamoja na kufananishwa na mkristo aliyeamua kubadili mwenedo kwa kuyaacha yale ya zamani bado hatuachi kusimama na kauli ya kuwatambua kwa matendo yao ni wangapi wanajiita wameokoka na kufungua makanisa kwa matangazo ya kufanya kazi ya Bwana lakini ukweli kazi yao kuu inakuwa wamebadili mfumo wa kupata pesa badala ya kuvamia na bunduki sasa atapokea sadaka kapuni. Na aje kama mwanachama asikimbilie kuomba/ombwa kuongoza.

@Karibu sana Ole Millya ... lakini uje kama mwananchama ... usituletee majigambo cha magamba. Uwe mwanachama, usaidie kujenga nguvu ya CHADEMA kutoka chini, mitaani, vijijni, hadi kieleweke. Baada ya hapo bila shaka waweza kugombea uongozi, lakini ..... kazi kwanza

@Nenda Millya Nenda,
Huko nako,
Chama cha wanatanzania,
Nao wanaitetea tanzania,
Mazuri na mema wayapigania.

Ukishafika huko,
Hizo pupa hebu achilia,
Nao pia hawatazivumilia,
Badilika uwe kiongozi tunayemfikilia, Madudu ya Julius Malema mbali utayatupilia,
Ngebe kwa viongozi shimoni utazishindilia,
Siha na tabia njema utaipalilia.

Tanzania oyeee


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.