ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 17, 2012

PICHA ZA TITANIC USHAHIDI TOSHA WA MABAKI YA ABIRIA WALIOPOTEZA MAISHA 100 YRS ILIYOPITA

A newly released photo from the North Atlantic site of the shipwrecked RMS Titanic shows evidence of human remains, federal officials are saying.Kupitia Uchunguzi uliofanywa katika kuadhimisha miaka 100 tangu kuzama kwake na picha zake zikionyeshwa hadharani na kutoa majibu, baadhi ya picha zinaonyesha koti na viatu pea kamili vikiwa vimezikwa katika tope zito kwenye eneo ambalo abiria hao waokufa kishaujaa na miili yao kuzama umbali wa maili mbili na nusu chini ya usawa wa bahari.

Titanic meli iliyokuwa na uzito wa tani 46,328 urefu mita 269, kina chake mita 10.5 yenye mbio kilomita 26 kwa saa hadi 44 kwa saa na yenye uwezo wa kubeba idadi ya abiria zaidi ya 3000 ilipata ajali kisha kuzama na maelfu ya abiria na mali zao mara baada ya kugonga mwamba wa barafu tarehe 13 1pril 1912 ikifanya safari kutoka Southampton nchini Uingereza kuelekea New York nchini Marekani.

Dr. James P. Delgado (PICHANI), ambaye ni mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Masuala ya majini, Maritime Heritage Museum toka Chombo cha Kitaifa cha Utawala wa Anga na Bahari (National Oceanic and Atmosphere Administration) kwa njia ya simu ameiambia Yahoo News kwamba jinsi viatu vimeweza kukutwa mahali pamoja inatengeneza picha halisi ya mlingano "compelling case" kwamba vilikuwa vinamilikiwa na mwili wa mtu uliolala miaka mia iliyopita mahali hapo.

Wataalamu hao wanasema kuwa wameiona picha halisi ya meli hiyo ikiwa chini ya maji ikiwa imegubikwa na tope jingi wakiongeza wanauhakika kuwa chombo hicho kitakuwa bado kina mabaki ya abiria wengi na vingi vya ushahidi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.