ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 18, 2012

WAWAKILISHI WA TANZANIA BUNGE LA E.A

VIGOGO kadhaa katika siasa za Tanzania, Makongoro Nyerere na Adam Kimbisa, ni miongoni mwa washindi wa nafasi ya ubunge kuwakilisha katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa miaka mitano ijayo.Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe(kushoto) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakipiga kura kuchagua wagombea wa ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki , mjini Dodoma. Kulia kwa Mbowe ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Kabwe Zitto. (Picha na Mohammed Mambo).

Kimbisa aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na Makongoro ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, waliibuka washindi katika uchaguzi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu ambao ulifanywa jana na wabunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania linaloendelea na Mkutano wa Saba mjini hapa.

Washindi wengine ni pamoja na Angela Kizigha, Abdullah Ali Hassan Mwinyi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCCA), Bernard Murunya mwenye.

Makongoro ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yu mmoja kati ya washindi, wengine ni Dk. Edmund Mndolwa, Elibariki Kingu, Evans Rweikiza, Mrisho Gambo, Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga, mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, William Malecela wote wa CCM na John Lifa-Chipaka (TADEA).

Shy-Rose (pichani kushoto) ambaye aliwahi kuwania nafasi hiyo miaka ya nyuma bila mafanikio, hatimaye ameibuka katika kundi la wanawake akishika nafasi ya pili nyuma ya Kizigha, kwa kupata kura 120. Kizigha alipata kura 166.

Kundi la Zanzibar, Abdullah ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, aliongoza kwa kupata kura 227 wakati mshindi mwingine Maryam Yahya Ussi alipata kura 91, huku vigogo kadhaa wakitupwa nje. Kwa upinzani, nafasi zimekwenda kwa Wakili maarufu, Twaha Taslima wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 175 na Nderakindo Kessy wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 113.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.