ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 29, 2012

KALUPILIPILI MA-, KALUCHUMVI MA-, INAKOLEA KWA SHINGO


Nakumbuka michezo niliyokuwa nikipenda kuidadisi na hata kutamani kuishiriki enzi za skuli moja wapo ni pamoja na mazingaombwe, wataalamu wa mambo wanasema ili uwe mwana mazingaombwe mzuri shurti uwe na roho ya 'UTHUBUTU' na hii ni kwa nia ya kuweza kufanikiwa kuteka hisia za watu (siunajuwa tena mambo ya kusimama mbele ya hadhira kama mshereheshaji lazima uwe na kitu cha ziada).

Maelezo zaidi  fanya chochote ambacho kitawafanya  wengine wakujadili wewe tu, kama pichani pale kati jamaa anajipika na vikorombwezo vya pishi akinyunyiza mwenyewe..... pembeni kuna akina sisi tukishangaa huku tukiwa na maswali mengi yasiyo kuwa na idadi na kicheko juu....

Namalizia hiviiiiiii:- "Kalupilipili ma-, kaluchumvi ma-, inakolea kwa shingo. Ni kwa wale tu wanaojua huu mziki, Chunguza mjomba utabaini" 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.