ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 29, 2012

PEP GUAARDIOLA LEAVING BARCELONA FULL PRESS CONFERENCE - 27 04 2012



Pamoja na Barcelona kuvunja rekodi ya mafanikio chini ya Pep Guardiola katika miaka minne iliyopita - akiiongoza timu hiyo kubeba jumala ya makombe 13 - msaidizi wake mkuu Tito Vilanova amekuwa mara nyingi hazungumziwi.

Mpaka leo, pindi kocha huyu mwenye miaka 42 alipoushangaza ulimwengu wa soka baada ya kuthibitishwa kwamba ndiye kocha atakayemrithi Guardiola na kuliongoza benchi la ufundi la Barcelona katika msimu ujao wa 2012-13.

Alizaliwa katika ukanda wa Catalan eneo la Bellcaire d'Emporda mwaka 1969, Vilanova amekuwa mtu wa karibu sana na kocha huyu wa sasa Blaugrana kwa wakati wote. Wawili hawa wamekuwa pamoja katika kituo cha La Masia katika miaka 1980s.

Lakini wakati Guardiola alipoenda na kuwa star katika kikosi cha Johan Cruyff -Dream Team - wakishinda makombe sita ya La Liga na moja la Ulaya katika miaka 11 - Vilanova alishindwa kuhitimu, na miaka miwili baada ya kukaa na kikosi cha Barcelona aliamua kuondoka na kwenda kucheza katika timu za Figueres, Celta Vigo, Badajoz, Mollorca, Lleida, Elche na Gramenet - ambapo aliamua kustaafu mwaka 2002, miaka 14 baada ya kuanza kucheza katika evel ya juu.

Vilanova baadae akaamua kuhamia katika ukocha. Experience kubwa zaidi ni pale alipokuwa mjurugenzi mkuu wa klabu ya daraja la 3 kuanzia mwaka 2006-07. Baadae akaamua kurudi Barcelona wakati kiangazi cha 2007 kama kocha msaidizi wa kikosicha Barca B chini ya Pep Guardiola. Wakati Guardiola alipomrithi Frank Rijkaard mwaka 2008, Vilanova alijiunga na Guardiola katika kikosi cha kwanza na kuwa kocha msaidizi katika kikosi cha kwanza cha Barcelona.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.