Sunday, April 29, 2012
Mchezaji wa timu ya Simba Mganda Emmanuel Okwi akikokota mpira kuelekea goli la timu ya Al Ahly Shandy, huku mchezaji wa timu ya Isaac Seun Malik wa timu ya Al- Shandy ya Sudan akijaribu kumzuia katika mchezo wa kombe la Shirikisho unaofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Simba, imefanikiwa kuitandika Al Shandy ya Sudan magoli 3-0 katika kipindi cha lala salama na kutoka kifua mbele katika mchezo huo wa kwanza kabla ya ule wa Sudan wiki mbili zijazo.
Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Patrick Mafisango, Uhuru Selemani na Emmanuel Okwi, hata hivyo mchezji Patrick Mafisango alikosa goli la penati baada ya mchezaji Emmanuel Okwi kuchezewa vibaya na beki wa timu ya Al Ahly Shandy katika kipindi cha kwanza.
Mashabiki wa Simba wakishangilia huku wakiwa wameshika sanamu ya mnyama.
Kundi la ushangiliaji la Mpira Pesa kutoka Magomeni kama ilivyo ada yake lilishangilia kwa nguvu na kutia hamasa ya mchezo huo.
HABARI /PICHA kwa hisani ya www.fullshangwe.blogspot.com
Tupe maoni yako
ni kawaida yetu wana msimbazi. hatujazoea kufungwa na waarabu... simba atakua bingwa wa mashindano haya inshallah
ReplyDelete