ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 29, 2012

UNYANYASAJI WA TRAFIC WASABABISHA DALADALA MWANZA KUGOMA LEO WASEMA MADEREVA

Wakazi wa jiji la Mwanza leo wamelazimika kutembea kwa miguu mara baada ya madreva wa mabasi madogo maarufu kwa jina la daladala kugoma wakishinikiza dreva mwenzao aliyewekwa lockup' aachiwe huru, kwani imekuwa kawaida sasa kwa wasimamizi hao wa usalama barabarani (matrafiki) kuwanyanyasa madreva na makonda kwa kuwabandikia makosa.

Pia madereva hao wamelalamikia ushuru wa zaidi ya shilingi 6,500/= kwa siku yaani tozo la shilingi 500/= kwa kwenda na kurudi 500/= sawasawa na shilingi 1,000/= kila safari, badala ya shilingi 500/= kwa siku kama inavyofanyika mikoa mingine.

Wamiliki wa Dalada wakiwa wamepaki vyombo vyao vya usafiri mbele ya ofisi za wilaya uwanja wa Ghand Hall kusubiri mkutano na RTO.

Bodaboda leo imekuwa siku kuu kwao...hapa ni katika kituo cha mahakamahi barabara ya Makongoro.

Dereva aliyeswekwa lockup' tangu jana bwana Protas B Son, baada ya soo kuwa kubwa ameachiwa kinyemela bila dhamana leo alfajiri mara baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kuwa kuna mgomo umeandaliwa kufanyika kuanzia leo.

Mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala kanda ya ziwa Protas Dede amewaomba radhi wananchi kwa hali iliyotokeza na usumbufu walioupata kwani imewabidi kutetea haki ili mambo yaende sawa.

Huu ndiyo usafiri wa leo.

Notifikesheni kwa kuning'iniza miguu nje sijui ni kwa style gani.

Ni notice namba 257 ya tarehe 26th August 2012 iliyotolewa tarehe 28march 2012 chukuchuku bila risiti.

Faini iliyotozwa kwa kosa la kuning'iniza miguu nje.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.