ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 21, 2012

KOZI YA MCHEZO WA NGUMI NI ZAMU YA MAKOCHA KUTUPIANA MASUMBWI

Kocha wa Tmu ya JKT, Saidi Omari 'Gogo Poa' (kushoto) wakioneshana ufundi wa kutupa makonde na Kocha wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' wakati wa mazoezi ya vitendo yanayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani leo kwenye kozi ya kimataifa ya mchezo wa ngumi.

Kocha mchezo wa ngumi wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' (kushoto) akitupiana makonde na kocha wa Mkoa wa Pwani, Gaudence Uyaga wakati wa mazoezi kwa vitendo kwa makocha hawo ambao wapo katika kozi ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi Duniani.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)


KOZI YA YA KIMATAIFA YA KUFUNDISHA MCHEZO WA NGUMI

Kozi ya Makocha wa Ngumi inayoendelea Kibaha, Pwani katika shule ya Filbart Bayi, inaendelea vema chini ya mkufunzi aliyeletwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Josef Diouf kutoka Senegal.

Ikiwa imefika siku ya sita makocha wanaohudhuria mafunzo hayo ya siku kumi, wamelizika na kiwango cha mkufunzi huyo kwa kusema kuwa mbinu za kiufundi na ujanja wa ufundishaji wa mchezo wa ngumi anazo wafundisha ni za kisasa na kwamba kwa sasa wameelewa msingi wa ufundishaji,hasa kwa kumwanzisha, kumwendeleza mchezaji hadi kufikia kuwa mchezaji wa kimataifa toufauti na awali ambapo walikuwa wanafundisha kwa mazoea bila kuwa na mbinu za kuwafanya wachezaji ili kuleta upinzani hasa katika mashindano ya kimataifa.

Lakini pia wamejifunza namna ya kuandaa ratiba za ufundishaji za siku kwa siku, wiki, mwezi na ratiba ya mashindano yanayowakabili

Kwa kujigamba Makocha kutoka mikoani wamesema ujuzi wao wataanza kuonyesha katika mashindano ya Taifa yatakayofanyika katikati ya mwezi wa February ya kuwa kutakuwa na ushindani mkali sana hasa kwa kuzingatia mikoa mingi makocha wake wamepata mafunzo hayo,na sasa timu za vyombo vya ulinzi na usalama na zile za Dar es salaam ziwe tayari kupata upinzani wa hali ya juu kwa kuwa sasa hata vilabu vya kutoka mikoani pia zina mbinu na ujanja wa ufundishaji kulingana na mabadiliko ya mchezo wa Ngumi Duniani.

Kozi hiyo inatazamiwa kumalizika tarehe 24/01/2012 na walimu watakaokuwa wamefaulu watatunukiwa vyeti vya kimataifa vya daraja la kwanza(level 1) na kuingizwa katika Database za Chama cha Ngumi cha Dunia AIBA na kwamba watakuwana haki ya kufundisha mchezo wa Ngumi popote Duniani

Wakati huo BFT kwa masikitiko makubwa inasikitika kupatwa na msiba wa bondia wa timu ya Taifa Godfrey Mbunda aliyefariki kwa kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki maeneo ya mbezi. Hakika hili ni pigo kubwa katika medani ya mchezo wa ngumi kwa kuwa bado mchango wake ulikuwa unahitajika kwa suala la maendeleo ya mchezo wa ngumi Tanzania

Makore Mashaga
KATIBU MKUU

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.