ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 13, 2012

HASIRA ZA MPANGAJI

MPENZI WA RIWAYA:
BAADA ya kufanya utafiti wa kina juu ya uhusiano uliopo kati ya mwenye nyumba na mpangaji, nikianzia Songea 2005 na kumalizia Mwanza 2011, sasa nakuletea riwaya ya kisayansi(science fiction).
HASIRA ZA MPANGAJI ni riwaya iliyotungwa na mimi Gabriel Nombo. Inaelezea maisha ya watu kwenye sayari iliyo nje ya mfumo wa jua, extrasolar planet. Sayari yenye watu wanaopanga na wanaopangisha nyumba kama watu wa hapa duniani. Tofauti ni kwamba, wao wameendelea zaidi kisayansi na kiteknolojia ukilinganisha na sisi wa duniani.

Pia, kwa asili binadamu wa huko (aliens) wana hasira sana. Kwenye nyumba wanazoishi mifarakano ipo muda wote. Kitu kidogo tu, kwa wao, chaweza zua hasira kubwa.
Tafadhali usiikose riwaya hii ya aina yake. Ipo njiani kukutembelea.

Kwa maoni au maswali, tafadhali nitumie barua pepe hapo chini.
mapigaby@yahoo.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.