Wakati wa kuazimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Jijini London Ubalozi wetu katika siku ya Ijumaa Tarehe 9 Desemba 2011 ulipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.
Balozi Kallaghe, Tim, Semu Naibu Balozi Chabaka na Allen
Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi.
Tim Hunt na Frank Eyembe
Baraka Baraka Akifanya Mahojiano na afisa Semu.
Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.
Tim Hunt Reginal Manager Africa & Middle East
Kutoka Kushoto Naibu Balozi Chabaka, Semu na Tim
URBAN PULSE CREATIVE & Miss Jestina Blog
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.