ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 27, 2011

MISS TOURISM MARA 2011 NASEMA SIKOSI NG'OO!

Hatimaye lile shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Mara katika maswala ya utalii, litafanyika Ijumaa ya tarehe 07/10/2011, katika ukumbi wa Bwalo la Magereza mjini Musoma, ambapo takriban warembo 15 watapanda jukwaa moja kuchuana kumpata muakilishi wa mkoa katika mashindano yan Miss Tourism Lake Zone yatakayofanyika baadae mwezi december.

Kampuni ya Stoppers Entertainment inayoandaa mashindano hayo, imejipanga kuyapa hadhi mashindano hayo ambapo warembo mbali na kupita jukwaani, watashiriki katika shughuli za kijamii, kuimba na kucheza ngoma za makabila ya mkoa wa Mara.

Hata hivyo waandaji wamewaomba wadhamini kuendelea kujitokeza kudhamini shindano hilo, kutokana na kugusa utalii, utamaduni na uchumi wa nchi yetu, yote kwa minaajili ya kuitangaza Tanzania.

Shindano la Miss Tourism Mara 2011, litasindikizwa na burudani kutoka kwa Ditto na Linah wote kutoka jumba la vipaji THT. Pia burudani za ngoma za asili zitakuwepo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.