ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 26, 2011

BASHE ASHIKA KAPU KUMUUNGA MKONO DIWANI KATA YA MKOLANI KUCHANGIA MAENDELEO

Mgeni rasmi wa ufunguzi Michuano ya mkolani Cup Hussein Bashe akipokea mchango toka kwa mtoto Elizabeth aliyeguswa kuchangia maendeleo ya kata ya mkolani fedha hizo kutumika kujenga madarasa pamoja na nyumba za walimu.

Mafundi Fc katika picha ya pamoja.

Kikosi machachari cha Mkolani Fc

Marafiki mbalimbali wa Mh. Diwani Stanslaus Mabula nao hawakuwa nyuma kumsapoti katika hili alilolianzisha kwa maendeleo ya kata ya Mkolani, pichani mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza Jack Fish akitoa mchango wake kwenye kapu kama ongezo kwa ahadi aliyoitoa.

Mashindano ya mpira wa miguu na mikono ya kombe la diwani kata ya Mkolani yajulikanayo MKOLANI CUP 2011 yamekwisha zinduliwa rasmi jijini Mwanza nayo yataendelea kwa siku 40 tangu sasa.


Timu 16 kutoka mitaa ya kata hiyo inashiriki kwa mtindo wa ligi na kisha kupatikana timu 8 bora zitakazocheza hadi kupatikana mshindi wa mashindano hayo.

Mshike mshike mchezo baina ya Mkolani Fc na Mafundi Fc.

Mchezo huu wa ufunguzi ilibidi uhairishwe katika dakika ya 20 kipindi cha pili kutokana na kiza kuingia kwani watu walitumia muda mwingi kuchangia mfuko wa maendeleo, mchezo umepangwa kurudiwa tena.

Kosakosa langoni mwa Mkolani Fc ambao mpaka mchezo unaahirishwa walikuwa wakiongoza kwa bao moja bila.

Safu ya marafiki wa Mh. diwani waliofika kusapoti maendeleo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.