AU ilisema kwenye taarifa yake kwamba amri hiyo inatatanisha sana juhudi za mataifa ya Afrika za kutafuta suluhu ya kisiasa katika vita vya Libya.
Mkuu wa AU, Jean Ping, alisema siyo kwamba viongozi wa Afrika wako dhidi ya ICC, lakini wanaona kuwa mahakama hayo yanawalenga wakuu wa Afrika tu.
Pichani: Obama akiwa na Kanali Gaddafi.
Alimuelezea Mkuu wa Mashtaka wa ICC, Luis Moreno Ocampo, kuwa "mzaha" ("a joke""). Wakati huo huo, wawakilishi wa wapiganaji wa Libya, walikaribisha mpango wa AU wa kufanya mazungumzo bila ya Kanali Gaddafi kuhudhuria.
Hilo linaweza kuwa fanikio la mwanzo la AU kuhusu Libya, ambayo kabla ikionesha kama imegawika juu ya swala hilo.
Kwa hisani ya bbc swahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.