ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 15, 2011

CHELSEA STAR DIDIER DROGBA'S WEDDING IN PICTURES

Mwishoni mwa wiki mkali wa soka toka Ivory Coast anayekiputa klabu ya Chelsea ya London nchini Uingereza, Didier Drogba amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi waliozaa nae watoto watatu aitwae Lalla Diakite huko Marie De monaco nchini Ufaransa.

Sherehe hiyo ilisimamiwa na mnene wa Chelsea Roman Abramovich, huku wachezaji mwenzake Salomon Kalou na Florent Malouda wakisimama katika nafasi ya upambe.

Wageni walioalikwa ni pamoja na mkali wa Rnb Akon star wa tumbuizo za NBA pia alimuita msanii anayemzimia kinomanoma Fally Ipupa toka Congo-DRC na J.Martins toka Nigeria.


Long-term love: Drogba na mke wake aliyefunga nae ndoa mwishoni mwa wiki hapa ilikuwa ni katika moja ya pati iliyofanyika jiji la London nchini Uingereza mwezi September mwaka jana.

Wapenyezaji habari wamenena kuwa: ‘Drogba anaupenda sana wimbo Jupa Remix na alikuwa akidhani ni wa Fally Ipupa’ ‘hivyo alipomkaribia Fally kumtaka awepo iliapate kuperform kwa harusi hiyo kama wimbo maalum, alimjibu kuwa hilo songi si lake. Na iliapate kuliperform kwenye sherehe ya ndoa hiyo kwa ufanisi zaidi haina budi kuwasiliana na mchizi aliyempa kolabo J.Martins (the owner of the song) awepo shughulini na wimbo upate imbwa’. Drogba alifanya hivyo na songi likagengeshwa kunako shughulini.


Kwahisani ya indepthafrica.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.