Daraja hilo la Mto Malagarasi linalounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora lililokwama tangu uhuru, ujenzi wake utakagharimu dola za Marekani milioni 56. Mradi huo pia unajumuisha ujenzi wa kilometa 48 za barabara ya kiwango cha lami.
Meneja huyo amesema tayari kampuni yake imeoneshwa eneo la mradi na ameanza kufanya kazi hiyo ya ujenzi inayojumuisha madaraja matatu yenye urefu wa meta 200, meta 50 na meta 25.
Mradi huo uliosainiwa Oktoba 22, 2010 utachukua miezi 36 kukamilika na mkandarasi amekabidhiwa eneo la kazi Desemba 10, 2010 na kwa sasa anajipanga kujenga kambi ili kuanza ujenzi.
Wakati ujenzi wa daraja hilo ukianza, mawasiliano kati ya Kigoma na Tabora kupitia bonde la mto huo yamekatika baada ya kujaa maji na kusababisha magari kuishia upande mmoja wa barabara na abiria kulazimika kupita kwa miguu juu ya daraja la treni na kupanda gari linguine upande wa pili.
Sambamba na ujenzi wa daraja hilo, Menea huyo alisema ujenzi wa barabara ya Kidahwe – Uvinza kwa kiwango cha lami kwa urefu wa kilometa 76.6, unaogharimu Sh bilioni 78.2 tayari nao umekwishaanza chini ya utekelezaji wa kampuni ya CHICCO kutoka China na Mhandisi Mshauri, Kampuni ya International Consultants and Technocrats Pvt Ltd. ya India.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.