Akizungumza na blog hili, mraribu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema tayari wamejiandaa vyema kwa ajili ya kufanya uzinduzi huo na mashindano hayo rasmi yatafanyika Mei 13 katika Ukumbi wa Triple A jijini humo.
Mpaka sasa wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha. "Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni uzinduzi wa mashindano hayo ili tuweze kuendelea na kila kitu," alisema Bi. Sophia Urio.
Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.
Wadhamini katika shindano hilo ni Vodacom, Startimes, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.