Anaaminika kuwa ndiye mtu aliyeagizwa kufanyika kwa mashambulio yaliyotokea New York na Washington, Septemba 11 mwaka 2001, pamoja na mashambulio mengi kadhaa ya mabomu yaliyosababisha vifo. Alikuwa ndiye mtu anayesakwa zaidi duniani. Lakini maelezo yake katika orodha hiyo yamebadilishwa na sasa kuna sehemu inasomeka: "Amefariki".UHAKIKA
Vipimo vya DNA vilivyofanywa baada ya harakati hiyo vinaonyesha kwa uhakika wa asilimia "99.9%" kuwa mtu aliyepigwa risasi ni Osama Bin Laden, maafisa wa Marekani walieleza.
Maafisa wa wizara ya ulinzi wanaeleza kuwa alizikwa baharini baada ya kuswaliwa kwa mujibu wa taratibu za kiislamu kwenye meli ya kubebe ndege katika bahari ya Arabuni.
Marekani imeweka ofisi zake katika hali ya tahadhari kote duniani, ikiwaonya raia wake kuhusu uwezekano wa mashambulio ya al-Qaeda kulipiza kisasi kwa kifo cha Bin Laden. Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la CIA, Leon Panetta, amesema al-Qaeda kuna uwezekano mkubwa kujaribu kulipiza kwa yaliyotokea.
kwa hisani ya bbc.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.