Boti zilizotengenezwa kwa ajili ya doria bahari ya hindi na Kampuni ya uundaji wa boti ya Songoro Marine Transport Ltd ya jijini Mwanza zimekamilika na tayari zimekabidhiwa kwa kampuni ya doria ijulikanayo kwa jina la Marine & Coastal Environment Management Project (MACEMP) tayari kwa kutoa huduma.
Mafundi wa Songoro marine Transport Ltd wanavyokuwa kazini.
Boti hizo zitakazo kwenda kufanya kazi ya doria bahari ya hindi mara baada ya kufanyiwa ukaguzi na kuonekana kuwa na viwango vya ubora kufanya safari zake baharini muda wowote kuanzia sasa zitasafirishwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara zikiwa tayari zimehakikiwa kwa viwango vya usalama barabarani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment