Ingawa Inatajwa kuwa kuna ukuaji wa kasi wa Masoko katika nchi za Afrika Mashariki, elimu kwa soko la mtaji inaonekana kuwa kikwazo kikubwa kufanikisha suala zima la Uwekezaji.
Hayo yamebainishwa leo katika ripoti ya mwaka ya mkutano wa siku mbili wa muungano wa soko la hisa Afrika uliomalizika leo katika hoteli ya Malaika jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi wa masoko wa nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na wenyeji Tanzania.
MAAZIMO mbalimbali yamefikiwa ikiwa ni pamoja na
-Kuandaa miongozo itakayowezesha wawekezaji kujumuika pamoja.
-Kuweka mikakati kurahisisha fursa za uwekezaji katika nchi husika kutoka soko linalouza hadi soko linalonunua.
WAKATI mkutano huu ukifanyika na Tanzania kuwa wenyeji takwimu zinaonyesha idadi ya watanzania waliowekeza hadi sasa kupitia hisa za kampuni zilizorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es salaam – DSE, ni ndogo mno jambo linalobainisha kuwa ushiriki wa watanzania katika kujenga uchumi wa nchi yao baada ya serikali kujiondoa katika biashara na kuruhusu sekta binafsi kuendesha uchumi ni mdogo sana, kiashiria tosha kwamba serikali inalojukumu kuelimisha umma faida za uwekezaji katika Hisa kabla ya soko hilo kutekwa na wananchi wa nchi nyingine za jumuia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.