Bw Nelson Mandela ameenda nyumbani kwake kijijini mjini Eastern Cape nchini Afrika kusini katika safari yake ya kwanza tangu alipolazwa hospitalini mwezi Januari.Family Support: Nelson Mandela na binti yake Princes Zenani Mandela-Dlamini (shoto)na Mjukuu wake Ndileka Mandela picha ilipigwa mara baada ya Mzee Madiba kupiga kura nyumbani kwao.
Aliyekuwa rais wa nchi hiyo mwenye umri wa miaka 92 alitembelea Qunu akitokea mjini Johannesburg akiwa na kikosi cha madaktari.
Baada ya kuondoka uwanja wa ndege akisindikizwa na ujumbe wa magari 12, inasemwa yuko nyumbani kwake Qunu pamoja na mke wake.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma alisema "amefurahi kwamba sasa afya yake imeimarika kiasi cha kuweza kusafiri". Bw Mandela amekuwa akipata matibabu nyumbani kwake Johannesburg baada ya kutibiwa kutokana na matatizo ya moyo mapema mwaka huu.
Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel hajatokea hadharani tangu sherehe za kufunga mashindano ya kombe la dunia mjini Johannesburg Julai 2010.
WATANZANIA WATAKIWA KUULINDA MUUNGANO
-
*Na Oscar Assenga,TANGA*
*WATANZANIA wametakiwa kuendelea kuenzi na kuulinda Muungano uliopo hapa
nchini ambayo ni tunu kubwa ilioachiwa na Waasisi wa Tai...
”Rasmi Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba lavunjwa”
-
Soko Kuu la Manispaa Bukoba limevunjwa ili kupisha ujenzi wa soko jipya la
kimataifa unaotarajiwa kuanza muda wowote.
Kwa Wakati tofauti wameonekana Wafa...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.