Mbali ya kifungo hicho, pia wametakiwa kurudisha Sh1.8 bilioni walizochota kwenye akaunti hiyo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na endapo watashindwa kufanya hivyo, mali zao zitakamatwa na kufilisiwa.
Hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya saa mbili, ilisomwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ilvin Mgeta kwa niaba ya jopo la mahakimu watatu waliokuwa wakiisikiliza. Mahakimu wengine ni Focus Bampikya na Saul Kinemela.
Maranda na mwenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwamo ya kula njama, kughushi, wizi, kuwasilisha hati za uongo na kujipatia ingizo la fedha kwa njia ya udanganyifu kwenye akaunti kiasi cha Sh1.8 bilioni, mali ya BoT wakijaribu kuonyesha kuwa Kampuni yao ya Kiloloma & Brothers imepewa idhini ya kukusanya deni la Kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai, India.
Watuhumiwa wakipanda gari tayari kwa safari ya rumande.
WASHITAKIWA KUKATA RUFAA?
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo, Wakili Magafu alisema wateja wake hawajaridhika na hukumu hiyo, hivyo wataomba mwenendo mzima wa kesi hiyo ikiwamo hukumu ili waisome halafu watajua cha kufanya.
hisani ya mwananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.