


ZENGWE LA KABLA YA MPAMBANO.
Awali mechi hiyo iliingia doa la vimelea vya siasa kiasi cha kutaka kutokuchezwa kabisa, mara baada ya wamiliki wa uwanja huo wa CCM Kirumba (wakiwa tayari wamelipwa gharama zote za uwanja) walinzi wake waliweka ngumu kabisa bila sababu za msingi kufungua milango ya uwanja huo ili shughuli ipate kuanza kama ilivyokuwa makubaliano yaani saa 6:00, wakisubiri maelekezo toka kwa ngazi na ngazi. Kumbuka kuwa uwanja huu unamilikiwa na Chama cha mapinduzi (CCM) na Ilikuwa ni mechi iliyoandaliwa na Coco Intertainment ya jijini Mwanza, Mbunge wa Ilemela Mh. Highness Samson (CHADEMA) akiwa mgeni rasmi mahususi kuchangia ununuzi wa madawati Shule za msingi Wilaya ya Ilemela ambapo shule nyingi wanafunzi wanakalia matofali. Chekshia Hali ilivyokuwa:-
Tupe maoni yako
Isee!! poleni kwa yote yaliyotokea kuhusu kukataliwa kufunguliwa milango mapema.
ReplyDeleteIla hizo ni sababu zisizo za misingi, hata kama kiwanja kinamilikiwa na CCM wakumbuke kuwa viwanja vyote vimejengwa kwa nguvu ya wanainchi wote ila wakati huo ilikuwa ni chama kimoja.kuwepo kwa vyama vingi vya siasa hakumnyimi mtu yeyote haki ya kutumia kiwanja. mambo haya yanahitaji marekebisho.