ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 3, 2011

ROCK CITY STAR NA BONGO FLEVA NGOMA DROO.

Mchezo kati ya Bongo fleva fc na Rock City Star ya jijini Mwanza uliopigwa jana katika dimba la CCM Kirumba umemalizika kwa sare ya 2-2.

Mgeni rasmi wa mchezo huo Raphael Shilatu ambaye ni Afisa utawala wa Sahara Communication (Radio Free Africa, Star tv na Msanii Afrika) akisalimiana na wachezaji wa Rock city star.

Rock Star ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 20mfungaji akiwa kapteni Ally Coco na kisha la pili likatupiwa nae Nico Mkumbaile.

MAKAPTENI WA TIMU WAKIPEANA SALAAM.
Mashabiki wakiamini kuwa timu hizo zitaenda mapumziko kwa bongo fleva kulala mbili kavu hali haikuwa hivyo kwani kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Ben Kinyaiya aliizawadia Bongo Fleva bao la kwanza,

BONGO FLEVA FC.

Nacho kipindi cha pili dakika ya 23 Rock City Star ilibidi kucheza pungufu mara baada ya mara baada ya Jack Fish kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya Richie One
Walikuwa Bongo Fleva fc ndiyo waliopata bao la pili kupitia mchezaji wao mahiri H.Baba baada ya kupokea pasi safi toka kwake Kara Mura

Bongo Fleva Fc.

Rock City Star.
Hadi kipyenga cha mwisho kinalia timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 2-2.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Looks like you folks are having a lot fun.

    http://goo.gl/3UKz

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.