Tanesco walifika mapema eneo la tukio kukata umeme usilete madhara.
Kabla ya hatua hiyo iliyokuwa ikitishia amani inasemekana gari hilo lilifika hatua chache kuelekea eneo la tukio kisha dreva wake kudai kuwa gari lina maji ilalimeishiwa mafuta hivyo kushindwa kusogea eneo la nyumba inapoungua na kutoa msaada.
Pamoja na sababu hizo za zimamoto wananchi hawakubweteka kwani kwa kushirikiana na wafanyakazi wa moja ya gereji iliyokaribu na eneo la nyumba hiyo walifanikiwa kuuzimamoto huo ulioanza saa mbili asubuhi na hatimaye kuzimika kabisa saa nne na dakika 45.
Majibu ya wafanyakazi wa zimamoto kuwa gari lina maji ila limeishiwa mafuta kuwa ndiyo sababu pekee ya kushindwa kufanya kazi iliyopaswa yalithibitishwa na wananchi hao kwa kutaka kuchungulia matanki ya maji ya gari hilo ambapo walipewa ruksa.
Hasira zadi ziliwapanda wananchi hao mara baada ya kugundua kuwa gari hilo lilifika eneo hilo la moto kiushahidi tu huku likiwa halina hata tone la maji kiasi kwamba ilibidi jeshi la polisi kuingilia kati mara baada ya kupewa taarifa ya vurugu hizo na hatimaye kufika eneo la tukio kuwatuliza wananchi na kulinda amani.
Bomba la maji gari la zimamoto cheche empty...
Katika Zogo hilo wananchi waliibua matumizi mengine mbadala ya magari hayo ikiwa ni pamoja na kusomba maji kwaajili makampuni binafsi ya utengenezaji matofali, ujenzi pamoja na magari hayo hutumika kusomba maji na kuyapeleka machinjioni.
Kwa mujibu wa mpangaji wa nyumba hiyo bi Mariam Mohamed anadai kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme kwani alipokuwa sebuleni akiangalia luninga alisikia sauti ya kishindo cha mlipuko sambamba na kuona moshi mzito mweusi ukitokea koridoni na hatimaye moto kamili.
Bado haijatolewa thamani halisi na hasara kwa janga hilo la moto
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.