ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 23, 2011

TUJIANDAE NA CHANGA LA MACHO JINGINE.......

MNYONGE Mtanzania na zigo la Dowans kwa Tanesco katika mtazano wa Katuni.

Miliki wa Dowans, Suleiman Al Adawi ameibua mjadala mzito nchini tangu alipotua na kufanya mkutano na wahariri wa magazeti matano Jumapili iliyopita, akigoma kupigwa picha pia akizuia televisheni na redio, huku akificha sura yake na sauti. Hata hivyo, mbio hizo za Al Adawi kukwepa kamera za waandishi jana ziliishia ukingoni baada ya kunaswa na kamera za gazeti la Mwananchi wakati akikagua mali zake zilizopo Ubungo.

Mpango mkakati wa kumnasa Al Adawi, ulipangwa na kufanikishwa kwa pamoja na duru huru za habari kutoka kwa raia wema ambao, awali walidokeza kuwa bosi huyo wa Dowans angefanya ziara kukagua mitambo ya kampuni hiyo mapema asubuhi. Swali ni kwamba nini kitafuata baada ya hili....

Habari kamili tembelea mwananchi.co.tz

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.