ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 21, 2011

AJALI KASAMWA.

Hebu Angalia Ajali mbaya ilitokea tarehe 19/02/2011 maeneo ya Kasamwa njia kuu ya kwenda Geita na Mikoa ya Kagera na Kigoma ukitokea Mwanza.

Benz C class.
Kwa mazingira ya ajali inavyosomeka inaonekana kabisa dereva mwenye gari hili lenye namba za usajili RAB155K (No.za Rwanda) alimfuata dereva wa Rav4 na hatimaye kugongana nae uso kwa uso.

Toyota Rav4
Ajali hii mbaya imehusisha magari mawili kama yanavyoonekana pichani, Silver Mercedes Benz C class na Blue Toyota Rav 4

Ukiitizama Rav4 kwa nyuma salama salmini....!

Dereva wa Mercedes Benz alifariki dunia hapo hapo na abiria wa kwenye Rav 4 walifika Hosp wakiwa hoi na baadae kufariki

Bado hatujaelewa kama hiyo Benz kwa vile ina usajili wa Rwanda na kule kwa wenzetu wanatumia barabara kwa kuendeshea magari moto upande wa kulia, labda ndio sababu akajisahau!!.. Mh! maana huko kugongana ndio kunatatanisha.

Shukrani kwa taarifa na Picha @Alawi Mdee.

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.