ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 30, 2011

MMASAI AZUA KIZAA ZAA KAMBI YA MISS KISURA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mshiriki mmoja wa fainali za Miss Kisura Tanzania 2011, Kipoyane Laibon, kutoka mkoani Arusha, ameripoti kambini hapo akiwa sambamba na mumewe.Mrembo huyo akionyesha ishara ya upole uliopitiliza wakati akihojiwa na kujibu kwa kilugha huku akifinyafinya kucha zake, alisema kuwa, amefika mahala hapo kushiriki shindano la JITAMBUE KISURA, lakini hakuzoea kuwa mahala bila mumewe na ndiyo maana wameamua kusindikizana.

VISURA WAKIWASILI KAMBINI.

Mumewe huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, akiwaameongozana na Kaka wa mshiriki huyo, muda wote walionekana kambini hapo wakiwa na vijifurushi vyao wakiwa nje ya Hoteli hiyo waliyofikia warembo hao wakisubiri muafaka. Mumewe huyo alisema kuwa ameamua kumsindikiza na kuwaomba wahusika ili kupatiwa mahala pa kulala na mkewe huyo ikiwa ni moja ya kumlinda mkewe na kudumisha mila za kwao.MUME NA KAKA WA MSHIRIKI NJE YA HOTELI.
Bila wasiwasi wakizungumza kiswahili kwa taabu, angalau kuliko hata huyo mrembo mwenyewe, walisema kuwa, wamefika mahala hapo kumsindikiza mshiriki huyo, ambaye kamwe hawaamini kumuacha pekee.

HABARI NA PICHA KWA HISANI YA sufianimafoto.blogspot.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.