MGOMBEA WA URAIS KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), JAKAYA KIKWETE AMETANGAZWA RASMI KUWA MSHINDI WA UCHAGUZI WA RAIS WA TANZANIA ULIOFANYIKA JUMAPILI NA KUAPISHWA LEO MCHANA JIJINI DAR ES SALAAM.
BWANA KIKWETE AMEPATA JUMLA YA kura 5,276,827 AMBAZO NI SAWA NA ASILIMIA 61.17 YA KURA ZOTE ZILIZOPIGWA.
MGOMBEA WA CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), Dr WILBROD SLAA YUKO NAFASI YA PILI KWA KURA MILIONI MBILI NA LAKI MBILI, SAWA NA ASILIMIA 26.34.
PROFESA IBRAHIM LIPUMBA WA CUF, AMEAMBULIA NAFASI YA TATU BAADA YA KUJIKUSANYIA KURA 695,668 AMBAZO NI MGAO WA ASILIMIA NANE.
WAGOMBEA WENGINE NA ASILIMIA YA KURA ZAO NI PETER MZIRAY, ASILIMIA 1.12, HASHIM RUNGWE ASILIMIA 0.31, MUTAMWEGA MGAHYWA ASILIMIA 0.20 NA FAHMI DOVUTWA ASILIMIA 0.15.
BW KIKWETE AMEAPISHWA LEO KATIKA UWANJA WA UHURU KUTUMIKIA AWAMU YA PILI KAMA RAIS WA NNE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.